Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi katika ngazi mbalimbali za Serikali kuanza mara moja maandalizi ya kukabiliana na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha nchini katika kipindi kijacho.
Rais Samia amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Taasisi za Serikali kujiandaa mapema kukabiliana na uwezekano wa mvua kubwa zinazotabiriwa kunyesha nchini.