Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Zambia, Mutotwe Kafwaya, ameuawa wakati wa operesheni ya kiusalama katika eneo linalohusishwa na kiongozi wa upinzani, Brian Mundubile, polisi wamethibitisha.
Kifo hicho kimeongeza sintofahamu na wasiwasi wa kisiasa nchini humo kufuatia uchaguzi wa urais wa Agosti 13,2026.