Makamu wa Rais amesema hayo, wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Jengo la Dakhalia katika Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame iliyopo Kibuteni Unguja, Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra ya Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival 2026).
Amesema Dakhalia hiyo iliyofunguliwa ni sehemu ya miradi lukuki inayotekelezwa Zanzibar yenye lengo la kukuza na kuendeleza sekta ya elimu na kuifanya kuwa ya mfano wa kuigwa kupitia uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu, na miundombinu ya kisasa kote visiwani.