Alisema mjadala huo utajikita katika masuala mbalimbali yanayohusiana na bahari na rasilimali zake, pamoja na rasilimali zinazopatikana katika mito na maziwa, ambazo zina nafasi muhimu katika kuimarisha shughuli za kiuchumi na kuongeza kipato cha wananchi.
Kongamano hilo litajadili pia umuhimu wa kuhifadhi mazingira ya bahari na vyanzo vingine vya maji, akisisitiza kuwa matumizi ya rasilimali hizo yanapaswa kwenda sambamba na uhifadhi wa mazingira.