Mabadiliko hayo yametangazwa na Kampuni ya Vodacom kwa kushirikiana na Chama cha Baiskeli Tanzania (CHABATA), sambamba na uzinduzi wa mashindano mapya ya Vodacom Coastal Classic, mbio za kilomita 109 zinazolenga kuiweka Tanzania kwenye ramani ya kimataifa ya mchezo wa baiskeli.
Vodacom Tanzania inazindua mashindano makubwa ya baiskeli ya Vodacom Coastal Classic, yakihusisha mbio za kilomita 109 zitakazoshirikisha waendesha baiskeli wa kiume na wa kike.