Helios Towers has officially launched a modern Information and Communication Technology (ICT) laboratory at Katale Secondary School in Bukoba District, Kagera Region, as part of its community investment programme aimed at supporting education and digital development in Tanzania.
Kampuni ya Helios Towers imezindua rasmi maabara ya kisasa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika Shule ya Sekondari Katale iliyopo wilaya Bukoba mkoani Kagera, ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kurudisha fadhila kwa jamii kupitia uwekezaji katika sekta ya elimu na maendeleo ya kidijitali nchini Tanzania.
Kwa muda mrefu, wanafunzi wa shule hiyo walikuwa na kiu ya kujifunza kompyuta, sasa wamepata maabara ya kisasa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) yenye kompyuta 25, jambo ambalo limeibua matumaini mapya kwa wanafunzi wanaotamani kujifunza na kutumia teknolojia.