Mataifa mengine yenye nguvu duniani yameongeza ushirikiano wake na Afrika.
Wakati mataifa makubwa duniani yakizidisha ushindani wa ushawishi barani Afrika, serikali za Afrika zinazidi kutumia ushindani huo kama fursa ya kusukuma mbele maslahi yao ya kiuchumi na kimkakati, hali inayoonyesha mabadiliko makubwa katika nafasi ya Afrika kwenye diplomasia ya kimataifa.
