Profesa Kyaharara amesema Serikali pia inaendelea kuboresha miundombinu ya usafiri katika maeneo ya uzalishaji ili kurahisisha usafirishaji wa mazao kutoka mashambani hadi kwenye masoko ya ndani na nje ya maeneo ya uzalishaji.
Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa kuwekeza katika barabara, madaraja, vivuko, umeme wa REA na miundombinu ya mawasiliano ili kupunguza gharama za uzalishaji, kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na kuwapa wananchi taarifa sahihi za masoko zinazowaongezea tija.