Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema kaulimbiu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ya 'Tunalipa Jana' si kauli tu, bali inatekelezwa kwa vitendo na imeonyesha ukwasi wa Mfuko huo kupitia ulipaji wa mafao kwa wakati kwa wanachama wanaostaafu.
Sasa hivi tunakwenda na kampeni ya 'Tunalipa Jana', ambayo inawezeshwa na utunzaji mzuri wa kumbukumbu, matumizi ya PSSSF Kidijitali na uwezo wa kifedha ambao Mfuko unao.