Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema uhitaji wa huduma za matibabu ya moyo nchini Comoro ni mkubwa kutokana na mwitikio uliokuwepo wakati wa kambi ya matibabu iliyofanyika mwezi Oktoba mwaka jana katika kisiwa cha Anjouan.
Dk Kisenge amesema mwitikio mkubwa wa wananchi wakati wa kambi hiyo umeonyesha kuwa mahitaji ya huduma za moyo nchini Comoro ni makubwa.