Kwa upande mwingine, ziara yake nchini Marekani imeonywa na Hezbollah, ambapo kundi hilo limesema Rais Aoun anaitafutia matatizo Lebanon.
Fayyad ameeleza kuwa Serikali ya Lebanon inataka maridhiano na Israel kana kwamba haioni uharibifu mkubwa uliofanywa na Taifa hilo nchini kwao. “Ni kama hakuna kilichotokea,” amesema Fayyad, akilenga hatua ya Israel kuteka eneo lote la Kusini mwa Lebanon.