Halmashauri imeweka mkazo katika kuwapatia wananchi elimu ya kitaalamu kuhusu uzalishaji bora, matumizi ya teknolojia, masoko ya mazao, kuongeza thamani ya bidhaa pamoja na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Jijini Dodoma.
Amesema ushiriki wa JKT, kupitia taasisi zake ikiwemo SUMA JKT, unalenga kuwajengea wananchi uelewa wa mbinu bora za uzalishaji katika sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi, pamoja na kuwaonesha fursa mbalimbali zinazoweza kuwainua kiuchumi.