Dk. Nguvila amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mfumo wa ununuzi wa umma ili kuongeza uwazi, kupunguza gharama za ununuzi, kuharakisha mchakato na kurahisisha ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma.
Dkt. Toba Nguvila amesema sekta ya ununuzi wa umma inahusisha sehemu kubwa ya matumizi ya fedha za serikali, hivyo kuna ulazima wa kuhakikisha fedha zote zinazotengwa zinasimamiwa kwa umakini mkubwa ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa.