Tume ya Ushindani (FCC) imetajwa kuwa mdau muhimu katika kuongeza thamani ya mazao ya Watanzania kupitia elimu ya ushindani wa haki na ulinzi wa mlaji, hatua inayowasaidia wazalishaji na wafanyabiashara kuboresha ubora wa bidhaa zao na kuzifanya zishindane katika masoko ya ndani na kimataifa.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, amesema Tume ya Ushindani (FCC) ina mchango mkubwa katika kuongeza thamani ya mazao ya Watanzania kupitia utoaji wa elimu kuhusu ushindani wa haki na ulinzi wa mlaji, jambo linalowasaidia wazalishaji na wafanyabiashara kuboresha ubora wa bidhaa zao na kuongeza ushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.