IFM imeeleza kuwa maonesho hayo yamejikita katika kuongeza thamani ya mazao na bidhaa ili ziweze kupata masoko yenye tija, ambapo ujuzi wa usimamizi wa fedha ni muhimu katika kuhakikisha mnyororo mzima wa thamani unakuwa na tija kwa wazalishaji.
Chuo hicho kimesema pale mazao yanapoingia sokoni, masuala ya usimamizi wa fedha huwa muhimu katika kuhakikisha wakulima wanapata mapato yanayoendana na thamani ya uzalishaji wao.