Dkt. Mollel amesema moja ya malengo ya Universal Medical Tourism ni kuendelea kuvutia wataalamu, teknolojia na uwekezaji wa afya kutoka nje ya nchi ili huduma nyingi zaidi zipatikane Tanzania.
Amesema kampuni hiyo pia inalenga kuendeleza ushirikiano kati ya madaktari wa Tanzania na wataalamu kutoka China kupitia kambi za matibabu na programu mbalimbali za kubadilishana ujuzi.