REDESO na VETA pia zimeandaa mtaala wa nishati safi ambao utaingizwa katika mitaala ya vyuo vya TVET vinavyoshiriki, ili kuhakikisha ujuzi kuhusu nishati safi unakuwa sehemu ya mafunzo ya kawaida ya ufundi stadi.
Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam wa VETA, Wilhard Soko amesema mafunzo hayo yanalenga kuandaa mitaala inayozingatia mahitaji ya soko la ajira na kuwawezesha vijana na wanawake kupata ajira katika sekta ya nishati jadidifu ndani na nje ya nchi.