Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), imefanya ziara ya ukaguzi katika mradi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko, kwa lengo la kujionea hatua ya utekelezaji wa mradi, kukagua miundombinu na maandalizi yaliyofanyika kuelekea kuanza kwa matumizi ya bandari hiyo, pamoja na kutathmini fursa zitakazotokana na uwekezaji huo katika shughuli za uvuvi na uchumi wa buluu.
Dkt. Kiula alisema TAFICO ni Shirika lenye uwezo wa kuchochea mnyororo mzima wa thamani wa sekta ya uvuvi, kuanzia uzalishaji hadi uchakataji na uongezaji thamani.