Amesema ushirikiano huo umeleta matokeo chanya ambapo wananchi wameendelea kushiriki katika shughuli za ulinzi na usalama, na kutoa taarifa zinazosaidia kuzuia uhalifu.
DCP Mwaibabe amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia viongozi hao kuelimisha wananchi, kuwajengea uwezo katika masuala ya ulinzi na usalama sambamba na kupambana na uhalifu.