Amesema kampeni ya “Linda Ushirika, Chagua Uadilifu” inalenga kuongeza uwazi, uwajibikaji na kupambana na vitendo vinavyoweza kudhoofisha maendeleo ya vyama vya ushirika nchini.
Vilevile, Serikali imewahimiza vyama vya ushirika kutumia kikamilifu fursa zilizopo katika masoko ya kikanda na kimataifa ili kuongeza thamani ya bidhaa na mapato ya wanachama, sambamba na kuendelea kutekeleza kampeni ya “Linda Ushirika, Chagua Uadilifu” inayolenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa na ubadhirifu.