Mhe. Kasaka alisema Chunya ina mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa kupitia uzalishaji wa dhahabu na tumbaku, huku akieleza kuwa wilaya hiyo inaongoza kwa uzalishaji wa dhahabu miongoni mwa wachimbaji wadogo nchini.
Mhe. Kasaka alisema utekelezaji wa miradi ya maendeleo na upatikanaji wa fedha kwa wakati ni muhimu katika kuongeza kasi ya shughuli za uzalishaji na kuimarisha uchumi wa Mkoa wa Mbeya.