Bima ya kilimo na ufugaji inasaidia wakulima na wafugaji kufanya shughuli zao kwa amani
Habari mpya za kilimo Tanzania · maelezo ya Bima ya kilimo na ufugaji inasaidia wakulima na wafugaj… · imesasishwa 10 Aug 2026 · habari za kilimo · wakulima · mazao
Muhtasari
- Amesema kwenye maonesho hayo Kijiji cha Bima kilipokea wageni zaidi ya 4,000 huku wengine wakiwafikia kupitia vyombo vya habari ambapo aliwasihi wananchi kufika katika ofisi mbalimbali za Bima kwaajili ya kupata elimu.
- Tunawasihi sana wananchi wawe na utaratibu wa kulinda shughuli zao za kilimo,ufugaji na uvuvi kwa kukata bima ambazo zitawasaidia pindi wanapokuwa wamepata majanga”,Amesema Isango Kwaupande wake Meneja wa Kanda ya Ziwa.
- Amesema kampuni hiyo inatoa bima ya kilimo na ufugaji ili kuwawezesha wakulima na wafugaji kufanya shughuli zao kwa amani huku wakijua kuwa wanaweza kufidiwa pale watakapopata majanga.
- Naye Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Kanda ya Ziwa, Stella Marwa alisema,shirika hilo linatoa bima za ajali na maisha ikiwemo bima ya kilimo inayomkinga mkulima dhidi ya ukame, wadudu, mvua nyingi na majanga.