na kutoa ramani ya kupata na kuanza mchakato wa Katiba mpya ya wananchi
Katika mapendekezo yake, chama hicho kimetaka kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kufutwa kwa kesi zinazodaiwa kuwa za kisiasa na ugaidi dhidi ya baadhi ya viongozi na wananchi, kuwepo kwa uwajibikaji kuhusu matukio ya uchaguzi wa mwaka 2025, pamoja na kuanzishwa kwa mazungumzo yatakayoshirikisha wapatanishi kutoka Umoja wa Afrika (AU) au SADC, ili kufungua njia ya kuhuishwa kwa mchakato wa Katiba Mpya.