Zaidi ya waoneshaji 500 wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wanatarajia kushiriki Maonesho ya 32 ya Kilimo na Mifugo na Sherehe za Wakulima Nanenane Kanda ya Kaskazini kwa kujikita kwenye kutambua soko, kuongeza tija na kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Maonesho ya 32 ya Kilimo na Mifugo na Sherehe za Wakulima Nanenane Kanda ya Kaskazini 2026, yatafunguliwa rasmi kesho rasmi tarehe 01 Agosti 2026, kwenye viwanja vya Themi Njiro Mkoani Arusha.
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha imesema imekamilisha maandalizi ya ushiriki wake katika Maonesho ya 32 ya Kilimo, Mifugo na Sherehe za Nanenane Kanda ya Kaskazini yanayoanza kesho, Agosti 1, 2026, huku ikisisitiza umuhimu wa wakulima kuongozwa na mahitaji ya soko ili kuongeza tija na kipato.
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha imejiandaa kushiriki Maonesho ya Wakulima na Wafugaji na Sherehe za Nanenane Kanda ya Kaskazini, yanayofanyika kuanzia Agosti Mosi hadi 09, 2026 katika viwanja vya Nanenane Themi Njiro jijini Arusha.