Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Bw. Denis Kwame Simba, aliwataka washiriki kutumia mifumo ya kielektroniki kwa ufanisi, kuzingatia uwazi, ushindani na thamani ya fedha, kutenga asilimia 30 ya zabuni kwa makundi maalum.
TARURA Tanga ilitambuliwa kwa kutekeleza kwa kiwango cha juu matakwa ya sheria yanayotaka asilimia 30 ya bajeti ya ununuzi kutengwa kwa ajili ya vikundi vya kijamii hatua iliyotajwa kuwa mfano bora wa utekelezaji wa sera za Serikali za kuwainua makundi yenye mahitaji maalum kiuchumi.