Misa hiyo inafanyika leo katika Kanisa Kuu la Kristu Mfalme, Jimbo Katoliki la Moshi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 tangu Askofu Minde alipowekwa wakfu kuwa askofu.
Maaskofu 20 washiriki Jubilee ya Miaka 25 ya Askofu Minde. Zaidi ya maaskofu 20 kutoka majimbo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania wamekusanyika katika Kanisa Kuu la Kristo Mfalme, Jimbo Katoliki la Moshi, kushiriki Masifu ya Jioni kuelekea maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25 ya Uaskofu wa Mhashamu Askofu Ludovick Joseph Minde.