Tira kuboresha huduma kidijitali

Serikali imeanza kutumia mifumo ya kidijitali kuboresha usimamizi wa sekta ya bima, ikiwamo kushughulikia malalamiko ya wateja na kudhibiti udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu katika soko hilo.