Katibu wa Tanzania Rugby Union (TRU), Bw. Anthony Dawa @elev8edtony, ametoa shukrani zake za dhati kuelekea kukuza mchezo nchini.

"Hatuhitaji misaada, tunahitaji ushirikiano wa kimkakati ambapo tukija pamoja tunaweza kuseti mipango itakayosaidia mchezo kukua."
— Anthony Dawa, Katibu Mkuu TRU
Mtangazaji (Interviewer):

"...ambavyo tayari mmeshazungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Waziri Mkuu Paul Makonda, umepata nafasi ya kuweza kukutana naye kwa maana kwamba ipo mikakati ambayo mmeizungumza tayari. Tunayo viongozi kuanzia ngazi ya juu ya serikali ambao sasa hivi wanasupport michezo mingi hapa Tanzania tofauti na miaka ya nyuma huko. Lakini sasa hivi mwamko umekuwa mkubwa kuweza kusupport kuhakikisha kwamba michezo hii inafanya vizuri. Nafasi ya wewe kama Katibu wa Shirikisho la mchezo huu hapa Tanzania, ni neno gani ambalo unalipeleka kwa viongozi wetu kuanzia ngazi ya juu ya serikali lakini pia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, wapo BMT, Rais wako Jacob pia Jonas ambaye umeizungumza kuhusiana na mchezo huu, kipi ambacho tunakihitaji, uwekezaji katika sehemu gani, kwa maana ya kutengeneza mchezo kuwa maarufu hapa Tanzania na kuweza kufikia huo ushindani wa kimataifa?"

Mgeni (Guest):

"Okay, so kwanza kabisa nitangulize shukrani kwa sababu ni wazi serikali inaonyesha nia ya kukuza sio mchezo tu wa rugby lakini michezo takriban yote hapa nchini. So kwa hilo tu niwaahidi pia hapo hapo kwamba wadau kama sisi hapa tupo tayari kuhakikisha michezo inakua nchini na tunaweza kufikia nyanja za juu kabisa. So kitu ambacho tunakihitaji sana sana saa hivi ni ushirikiano wa kimkakati. Sio misaada. Hatuhitaji misaada, tunahitaji ushirikiano wa kimkakati ambapo tukija pamoja tunaweza kuseti plans ambazo zitasaidia huu mchezo kukua na kuhakikisha vijana wanapata platform ambayo itawasaidia kujikimu sio tu kimaisha lakini pia kwenye... kwenye ins and outs za maisha yao daily, yaani kwenye daily life ile ambayo inaendelea hapa nchini. Hicho ndio kikubwa lakini vile vile ni kupata upenyo mkubwa zaidi wa kwenda kuupeleka huu mchezo mashuleni. Kwa sababu tunaamini vijana tunapowafikia kwa wingi zaidi ndipo ambapo huu mchezo unapata nafasi ya kutambulika na kupata umaarufu na pia vile vile tunapata nafasi ya kuidentify vipaji ambavyo tukivibroom ndivyo ambavyo vitaenda kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa."

💡 Mambo Muhimu ya Kufahamu

🤝

Ushirikiano wa Kimkakati

Lengo ni kujenga mifumo endelevu na mipango ya muda mrefu badala ya kutegemea misaada ya mara moja.

đŸĢ

Rugby Mashuleni

Kutumia shule kama kitovu cha kutambua na kukuza vipaji tangu umri mdogo ili kuimarisha timu za taifa.

🌱

Stadi za Maisha

Michezo inatoa platform kwa vijana kujikimu kimaisha na kupata ujuzi utakaowasaidia katika maisha ya kila siku.

Kipindi: SPORTS KIJIJI "michezo kiganjani mwako"
Host: @edgarmtawala6
Muda: 10:00 – 12:00 EAT
Tune on: www.mtawalaradio.online