NBC kuendelea kuwezesha wanawake, vijana katika kilimo

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeahidi kutekeleza mpango wa Serikali wa kuwawezesha wanawake na vijana katika mnyororo wa thamani wa kilimo, ikisema tayari imeanza kutoa huduma za kifedha kwa wakulima na vyama vya ushirika.