BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imewataka watanzania wanaopeana zawadi kwa njia ya kutunzana pesa taslimu katika sherehe mbalimbali nchini, waelekeze utaratibu huo kwa njia mifumo ya malipo ya kidijitali.

Hayo yamesemwa leo Agosti 4,2026 na Afisa Mwandamizi (BoT) Fredriki Mwakuu, alipokuwa akifanya mahojiano na NipasheDigital, mkoani Dodoma.

Mwakuu amesema kuwa kwa sasa serikali ipo katika malengo ya kupunguza matumizi ya pesa taslimu.

โ€œTunaona sasa hivi watu mbalimbali hususani akinamama wana tabia za kutunzana katika sherehe na kupelekea pesa kumwagika chini, ile haiko sawa BoT tumejipanga kuandaa mwongozo maalum kuhusiana na hilo,โ€ amefafanua

Mchambuzi Mwandamizi Mifumo ya Malipo ya Taifa (BOT) Doto Namkaa, amesema mifumo ya malipo imegawanyika katika malipo makubwa na madogo bila kujali matumiaji awe na akaunti yoyote kutoka benki.

Amefafanua mifumo ya malipo nchini itasaidia usalama wa wananchi kwa kuepukana na wizi, uhalifu pia kuzuia kutokuharibika kwa pesa na kuipa gharama BoT kwenda kuchapisha pesa zingine.

Amesema mifumo hiyo imekuja kurahisisha kuwawezesha wafanyabiashara, wakulima, wajasiriamali na wengine katika urahisishaji wa kazi zao.