Install nukta
Get the app experience on your phone.
nuktaai
SWEN
nuktaai
SWEN

Gundua

🌍 Gundua 📅 Matukio ⚽ Michezo ✈️ Safari Na Kuona 🍲 Chakula Na Kuonja 📊 Uchumi na Fedha 🌾 Bidhaa (Commodities) 💱 Fedha (Currencies) 👥 Matajiri Wamasoko 📂 Machapisho 📖 Kamusi / Tafsiri 🔬 Sayansi na Teknolojia 💼 Biashara 🎬 Burudani 🎮 Esports ℹ️ About

Habari Mpya

Kuhusu Msaada Privacy Terms
Social media
Instagram · Reel Siku 4 zilizopita

Imbeju Ndondo Cup 2026 ni mchongo, inategemea unaitazama kwa jicho gani! Wanao jiongeza tayari wameanza kufikiri nje ya box na kuzikamata fursa zitokanazo na u…

Clouds FM TZ

Nakala (transcript)

Woman: Sasa Ndondo Cup zinavyoanza hapa Chamazi zinatuletea fursa kwa ambao tunafanya biashara. Kwa sababu uwanja utajaa na sisi pia biashara tutafanya vizuri tu. Kama tulikuwa tunauza kilo mbili tutauza kilo tatu, umenielewa eh!

Interviewer: Na wewe unajishughulisha na biashara gani?

Woman: Mimi hapa nauza sambusa na kachori kwa sababu nawauzia watoto, ila kwa sababu ya Ndondo Cup inakuja itabidi nijiongeze zaidi. Badala ya watoto nawauzia na wakubwa yaani kama biashara itaongezeka.

Interviewer: Na Ndondo Cup msimu huu tunasema jiongeze.

Woman: Na jiongeze ndio maana yake, na maana ni kwamba ndio maana nimesema najiongeza, badala ya kuwauzia watoto kachori nitaweka na sambusa, nitaweka maandazi, na bila kusahau kahawa itakuwepo.

Interviewer: Sasa mechi ya ufunguzi itakusanya watu wengi sana, umejiandaa kiasi gani au utajiandaa kiasi gani kuhakikisha kwamba unaweza kutoa huduma kwa kundi kubwa la watu?

Woman: Nimejiandaa, fursa kama hii inavyokuwa inatokea lazima mtu ujiandae. Kivipi, kisaikolojia kwamba nahudumia watu wengi, ninavyokuwa nahudumia watu wengi na mimi nitakuwa peke yangu, lazima nimpe mtu pia fursa aje kunisaidia, ndio maana wenyewe wamenipa fursa na mimi natoa fursa.

Interviewer: Unawaambia nini wakina mama wengine ambao pia wanafanya biashara lakini huwa hawaji kwenye mechi ambazo zinahusisha mashindano ya Ndondo Cup?

Woman: Mimi nawakaribisha pia nawaambia waje kutazama Ndondo Cup na pia wajiongeze, yaani kwamba kujiongeza, wajishughulishe. Ndondo Cup inakusaidia wewe mwenyewe kutatua matatizo yako madogo madogo, tusitegemeane jamani, unakuwa umekaa nyumbani tu unamtegemea baba. Ndondo Cup ishaanza na haijaanza yaani sio kwamba inaanza siku moja inaisha siku moja, hapana. Inaweza ikatumia hata mwezi, ndani ya mwezi wewe hujafanya kitu, utakuwa umefanya kitu. Kwa hiyo mimi nawaambia wajiandae na Ndondo Cup tunawakaribisha.

Maelezo

Imbeju Ndondo Cup 2026 ni mchongo, inategemea unaitazama kwa jicho gani! Wanao jiongeza tayari wameanza kufikiri nje ya box na kuzikamata fursa zitokanazo na uwepo wa mashindano hayo kwenye maeneo yao.

Devotha Fikiri maarufu kama Mama God ni miongoni mwa wajasiriamali wanaofanya biashara zao pembeni ya uwanja wa Shule ya Msingi Chamazi ambao utatumika kwa mchezo wa ufunguzi wa hatua ya awali ya Imbeju Ndondo Cup 2026. Mechi hiyo kwake ni fursa ya kukimbiza biashara yake ya viburudisho.

Tukutane uwanja wa Shule ya Msingi Chamazi na ukitaka viburudisho vya kukuchangamsha wakati una-enjoy game mcheki mama God.

Machapisho asili

Angalia kwenye Instagram